Mbunge wa Viti Maalum, Ester Bulaya amesema anaamini chama anachokiwakilisha sasa bungeni ni Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza katika mahojiano maalum na Dar24 bungeni jijini Dodoma, Bulaya amesema kuwa suala la chama anachokiwakilisha liko wazi kwani asingekuwa na chama asingekuwa ndani ya nyumba hiyo ya wawakilishi.

“Hizo hazinisumbui kwa sababu ndio michezo ya kisiasa. Lakini kwa mtu ambaye anajua taratibu, hakuna mbunge anayeweza kuwa bungeni asiyekuwa na chama. Mimi ni mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),” amesema Ester Bulaya.  

Mbunge huyo pia amezungumzia kazi aliyoifanya Rais Samia na ushauri wake kwa Serikali, akimulika masuala ya ulipaji kodi ya nyumba kwa kutumia luku, upandishwaji wa bei za mafuta, miradi ya maji na kwanini alipiga kura ya kutokubali au kukataa.

Iangalie hapa kwa kina: