Kanuni na taratibu za kujenga hoja ndani ya Jumba la wawakilishi wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana zilimbana mbavu Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema), baada ya kutumia mfano tata dhidi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.

Bulaya alishauriwa kutumia maneno mazuri na yasiyo na dalili za udhalilishaji anapojenga hoja, baada ya kutoa mfano unaolenga kumfananisha Waziri huyo na mfano wa ‘tissue’.

“Mheshimiwa Maghembe, majibu yako yako ndiyo yatakayodhihirisha msemo wa Kinana kukuita wewe ni mzigo, lumbesa au ni mwepesi kama tissue,” alisema.

Kutokana na na kauli hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Jenista Mhagama aliomba utaratibu kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akikosoa kauli za mbunge huyo huku akimpa ushauri utakaomfaa.

“Namheshimu sana Mdogo wangu Esther, anaweza kujenga hoja vizuri, lakini usivunje kanuni, atumie maneno mazuri ambayo anaweza kufikisha ujumbe wake,” alisema Mhagama ambaye aliupigia mstari mfano wa ‘tissue’.

Bulaya alisimama na kujitetea akieleza kuwa neno hilo alilitumia kuonesha wepesi kama ulivyotumika mfano wa ‘mzigo’, lakini Mwenyekiti alimtaka kuketi kwani hakufuata utaratibu.

Video: Mbunge wa Mikumi Joseph Haule(Profesa Jay) afikisha kilio cha Mikumi Bungeni
SEKTA YA UMEME YANEEMEKA, MAKAMPUNI 52 YAJITOKEZA KUWEKEZA

Comments

comments