Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya anazidi kupeta dhidi ya mpinzani wake Stephen Wassira baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Ziwa kutupilia mbali kwa mara nyingine maombi ya wapambe wake kukata rufaa kupinga ushindi wake kupitia uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

ester bu

Maombi hayo yalikuwa yamewasilishwa mahakamani hapo na baadhi ya wapiga kura ambao ni wapambe wa Wassira, wakiiomba Mahakama kuwaruhusu kukata rufaa Mahakama ya Rufani baada ya kutoridhiswa na uamuzi wa awali.

Jaji Rose Ibrahim, ambaye anasikiliza shauri hilo la kupinga uchaguzi, alikubaliana na pingamizi lilolowekwa na wajibu maombi kuwa hayana mashiko kisheria.

Kupitia uchaguzi ulofanyika Oktoba 25 mwaka jana, Bulaya alipata ushindi wa kishindo wa kura 29,973 dhidi ya Wassira aliyepata kura 19,123.

Wassira alilalamikia matokeo hayo akidai kuwa uchaguzi uligubikwa na mapungufu makubwa pamoja na baadhi ya matokeo kupikwa.

 

 

 

Leicester City Hawakamatiki, Waendelea Kujichimbia Kileleni
Uliwahi kuipenda Hesabu? Leo ni siku ya Pie '22/7' duniani