Nchi za Kenya na Ethiopia zimekubaliana kuharakisha utekelezaji wa mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kiusalama ili kuweza kupambana na Ugaidi.

Nchi hizo zimekubaliana kuanzisha Tume ya Ushirikiano, ambayo ni muundo wa ngazi ya juu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Aidha, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa mzunguko wa bidhaa na watu kati ya nchi hizo mbili umeboreshwa kutokana na ujenzi wa kituo kimoja cha mpakani katika mji wa Moyale nchini Ethiopia.

“Napenda kutoa wito kuwepo msukumo mpya wa kuhakikisha hili linatekelezwa kwa mafanikio, kwa kuweka ratiba iliyo wazi na upatikanaji wa bidhaa zote katika hatua ya utekelezaji wa mkakati wetu,”amesema Kenyatta

Hata hivyo, Rais Kenyatta na Waziri Mkuu Abiy pia wamezungumzia mkakati wa nchi hizo mbili katika kupambana na ugaidi ambapo wametoa kipaumbele cha kurudisha utulivu Somalia na kushinda vita dhidi ya Al- Shabaab.

Kenya yaiva kisayansi kurusha satelaiti yake ya kwanza Japan
Masauni: Sio utaratibu Jeshi la Polisi kupiga raia, chukua hatua za kisheria