Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema leo kwamba amepeleka vikosi vya jeshi katika jimbo la Benishangul-Gumz magharibi mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya washambuliaji waliokuwa na bunduki kuwaua zaidi ya watu 100 katika eneo hilo, ambalo mara kwa mara hukumbwa na machafuko ya kikabila. 

Kituo cha televisheni kinachoegemea upande wa serikali Fana, kimetangaza kuwa jeshi la Ethiopia tayari limewaua watu 42 wenye silaha waliohusika na mauaji hayo. 

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali nchini humo, limeripoti kuwa maafisa watano wakuu katika jimbo hilo pia wametiwa nguvuni kuhusiana na masuala ya usalama wa eneo hilo. 

Jana Jumatano, tume ya haki za binadamu inayosimamiwa na serikali ilisema zaidi ya watu 100 waliuawa katika kijiji cha Bekoji kaunti ya Bulen ambako wakazi wake wengi ni mchanganyiko wa jamii mbalimbali. 

Watu kadhaa walioshuhudia mauaji hayo wamesema nyumba pia zilichomwa moto na watu wengine walidungwa na silaha zenye ncha kali.

Nigeria yaripoti aina mpya kirusi cha Corona
Wanaosafisha uchawi Sumbawanga waonywa