Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema kuna haja ya kusimamisha misaada ya chakula nchini humo kwakuwa inasababisha matatizo ya kiserikali.

Abiy amesema misaada hiyo imekua chanzo cha matatizo kwa kuwa ina mashinikizo mengi ya kigeni.

Ameongeza kuwa asilimia 70 ya matatizo ya Ethiopia yatasuluhika endapo misaada kutoka nje itakoma kwa kuwa inakuja na athari nyingi.

Taifa hilo linakabiliwa na shinikizo kutoka nchi kadhaa za magharibi kutokana na mzozo wa tigray ambapo mamilioni wapo katika hatari ya kukumbwa na njaa hivyo wakilazimika kupokea misaada ya chakula.

Kocha Gomes afichua siri ya kushinda ugenini
Tuchel: Mendy anastahili heshima