Serikali ya Ethiopia imetia saini muafaka wa amani na kundi moja la Waasi nchini humo la Oromo Liberation Front- OLF, ili kukomesha uhasama uliopo nchini humo.

Makubaliano hayo yametangazwa na Runinga ya taifa nchini Ethiopia ambapo mkataba huo umesainiwa katika mji mkuu wa Eritrea ambapo ndio makao makuu ya OLF.

Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa, sasa kundi hilo halitaitwa la kigaidi kama ilivyokuwa ikijulikana hapo awali.

Aidha, Waziri wa habari wa Eritrea, Yemane Gebremeskel amesema kuwa sasa OLF itatumia njia za amani kujishughulisha na masuala ya siasa nchini Ethiopia.

Hata hivyo, makubaliano hayo yanaonyesha hatua nyingine anayopiga Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed, ya kuzifanyia mabadiliko taasisi mbali mbali za taifa hilo, kupanua uchumi, pamoja na kuboresha usalama na uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine duniani.

 

 

Maafisa Madini wapewa somo utoaji wa leseni
Rais Kabila kuchukua maamuzi magumu