Shirika la Ndege la Ethiopia limesema kuwa limevisafirisha visanduku vya kurekodi kumbukumbu ya mawasiliano ya ndege au (black box) vya ndege ya Boeing 737 Max 8 iliyoanguka na kuwauwa watu 157 hadi Paris Ufaransa kwa uchunguzi.

Katika taarifa iliyoandikwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter wa shirika hilo, imesema kuwa ujumbe wa Ethiopia ukiongozwa na kitengo cha uchunguzi wa ajali AIB kimevipeleka visanduku hivyo huko Ufaransa.

Ethiopia imesema kuwa haina vifaa vya kusoma data zilizorekodiwa katika visanduku hivyo na Ujerumani imesema haitavifanyia uchunguzi visanduku hivyo kwa kuwa haiwezi kusoma mfumo wa kompyuta uliotumiwa na shirika la Boeing.

Mkuu wa Shirika la Mamlaka ya Anga la Marekani, FAA, Daniel Elwell amesema kuwa visanduku hivyo vya kurekodia data viliharibiwa katika ajali hiyo. Kulikuwa na kimya cha dakika moja nchini Kenya katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa One Planet ambao Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anahudhuria, kuwakumbuka waliofariki katika ajali hiyo.

Dawa za kutuliza maumivu hatari kwa figo, Dkt Ndugulile afunguka
CUF Ngangari! Timu Maalim yaliamsha kuhusu Uchaguzi wa Lipumba