Nahodha na Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon , Samuel Eto’o ametangaza kugombea Urais wa Shirikisho la soka nchini humo.

Eto’o amethibitisha kuwa kwenye mpango wa kuwania nafasi hiyo, kwa kuandika kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii.

Eto’o ameandika: “Nimeamua kuchukua uamuzi huu kwasababu ya kuipenda Cameroon na kupenda soka yetu…. ni wakati wa kujenga upya mpira wetu,” alielezea Eto’o katika taarifa yake hiyo.

Eto’o anaweza kukupambana na kizuizi kwa kile kinachodaiwa kuwa ana uraia pacha wa Hispania tangu wakati akicheza Barcelona.

Miongoni mwa masharti yanayotakiwa kuwa mgombea wa urais wa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon, ni marufuku ya kuwa na utaifa wa kigeni.

Samuel Eto’o ni kigogo wa tatu wa zamani kugombea urais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Cameroon. Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa ugombea wake utathibitishwa. Uchaguzi umepangwa kufanyika Desemba 11.

FC Barcelona kumpa muda Koeman
Mashabiki wa Arsenal waombwa kusubiri