Wajumbe wa Umoja wa Ulaya na Uingereza wanakutana leo Jumapili mjini Brussels katika mazungumzo yanayojaribu kufikia makubaliano ya kibiashara ya baada ya Brexit, huku maswala matatu muhimu yakisalia bado kizungumkuti.

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen na waziri mkuu wa Uingereza, Borris Johnson walifanya mazungumzo kwa njia ya simu siku ya Jumamosi na kuwaagiza wajumbe wao kuendelea
na mazungumzo katika jaribo la mwisho la kumaliza tofauti zilizoko.

“Tofauti kubwa bado zimesalia”, wamesema viongozi hao katika taarifa ya pamoja baada ya mazungumzo ya njia ya simu kutathmini uhusiano wa baadae wa Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Pande zote zimekiri kwamba muda unayoyoma wa kufikia makubaliano kabla ya kipindi cha mpito kumalizika mwishoni mwa mwaka huu. Viongozi hao wawili wamegusia pia maendeleo yaliyopatikana katika maeneo kadha lakini bado kuna mgawanyiko katika suala la haki za uvuvi.

Jonhson na Von der Leyen wamedai kuwa:

“Hakuna makubaliano yanayowezekana ikiwa tofauti juu ya masuala matatu muhimu ya utawala, uvuvi na kanuni za ushindani hayatapatiwa ufumbuzi,”.

Rais Magufuli amlilia jaji Nsekela
Marekani: Gavana wa Georgia ashinikizwa kupindua uchaguzi