Umoja wa Ulaya EU kupitia shirika la Maendeleo la Ufaransa AFD umeipatia Tanzania msaada wa shilingi Bilioni 84 kwa ajili ya mradi wa kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya Tanzania na Zambia.

Aidha sehemu ya fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 72 mkataba wake umesainiwa Desemba 15,2020, na Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na Mipango Doto James, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Fredric Clavier na Mkurugenzi Mkazi wa AFD Stephanie Essombe.

Katibu mkuu James, amesema kuwa kiasi cha fedha kitatumika kujenga kituo cha kupooza umeme Tunduma, kujenga njia ya kusafirisha umeme kv 330 yenye urefu wa kilometa 4 kutoka Tunduma hadi mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Amesema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa njia mpya ya kusafirishia umeme katika maeneno ya vijijini ambayo hayajafikiwa na Gridi ya Taifa na kuongeza uwezo wa njia zilizopo za kusafirishia umeme kupitia Iringa, Kisada, Mbeya, Tunduma na Sumbawanga.

Katwila kuipamba Ihefu FC dirisha dogo
Simiyu: Tarura yadai halmashauri Sh mil 130