Mchezaji bora wa karne ya 20, Edson Arantes do Nascimento (Pele) amemtaka mshambuliaji kinda wa timu ya taifa ya England na klabu ya Man Utd, Marcus Rashford kutohofia kuonyesha uwezo wake wote kupitia fainali za Euro 2016, ambazo zitaanza rasmi mwishoni mwa juma lijalo nchini Ufaransa.

Pele ametoa rai kwa mshambuliaji huyo, kwa kuamini Rashford ana uwezo mkubwa wa kucheza soka, hatua ambayo imemuwezesha kuwa sehemu ya kikosi cha timu yake ya taifa ni ujasiri alionao anapokua uwanjani.

Pale amesema ni bahati ilioje kwa kijana mdogo kama Rashford kuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambalo lina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kucheza nafasi ya ushambuliaji, tena kwa kuteuliwa kwenda kwenye fainali kubwa za barani Ulaya.

Amesema hadithi ya mshambuliaji huyo, inataka kufanana na ya kwake, pale alipoitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil akiwa na umri wa miaka 17 kwa ajili fainali za kombe la dunia za mwaka 1958.

Amesema alijaribu kutumia nafasi hiyo kwa kucheza kwa kujituma wakati wote na alimini ilikua ndio nafasi pekee ya kuudhihirishia ulimwengu kwamba, ana kipaji cha kucheza soka na katu hakubali kushindwa.

Kutokana na ujasiri aliouonyesha katika fainali za mwaka 1958, Pele amemtaka Rashford kuiga mfano huo na amemuhakikishia atafaulu na kufanikisha safari yake ya kuwa mchezaji mkubwa duniani kote.

Rashford, mwenye umri wa miaka 18, ameteuliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na klabu yake ya Man Utd msimu uliopita.

Hugo Lloris Agoma Kusaini Mkataba Mpya
Euro 2016: Graziano Pelle Azua Hofu Kambi Ya Italia