Shirikisho la Soka Barani Ulaya *UEFA* limeitoza faini timu ya taifa ya England, kufuatia mashabiki wa timu hiyo kummulika kwa tochi Mlinda Lango wa Denmark, Kasper Schmeichel.

UEFA imetangaza maamuzi hayo dhidi ya England, baada ya kujiridhisha kuwa Mashabiki wa The Three Lion walihusika na tukio hilo.

Pia UEFA imeionya England kwa tukio hilo kwa kusisitiza lisijirudie tena kwenye mchezo wa Fainali ambao watacheza dhidi ya Italia mwishoni mwa juma hili.

England waliifunga Denmark mabao 2-1 katika mchezo wa Nusu Fainali uliochezwa jana Jumatano (Julai 07),  Uwanja wa Wembley jijini London.

Italia ilitangulia Fainali juzi (Jumanne) kwa kuichapa Hispania kwa changamoto ya penati 4-2.

Timu hizo zilifikia hatua ya kupiga mikwaju ya penati,  baada ya kufungana bao 1-1 katika dakika 120,  Uwanja wa Wembley jijini London.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 9, 2021
Moses Phiri afunguka kutua Simba SC