Wachezaji Michael Carrick, Antonio Valencia pamoja na Matteo Darmian wameachwa mjini Manchester, wakati kikosi cha Mashetani Wekundi kiliposafiri kuelekea nchini Ukraine, tayari kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Europa League utakaochezwa hii leo dhidi ya Zorya Luhansk.
Kuachwa kwa wachezaji hao kumetokana na hali zao kiafya kutokua vyema na ushauri ambao ulitolewa na jopo la madaktari umeshinikiza wachezaji hao kuachwa ili wapate muda wa kupumzika.
Kikosi kilichosafiri kuelekea Ukraine yupo De Gea, Romero, Johnstone, Fosu-Mensah, Jones, Bailly, Rojo, Blind, Young, Fellaini, Herrera, Pogba, Lingard, Mata, Mkhitaryan, Martial, Rashford, Rooney na Ibrahimovic.
Kukosekana kwa wachezaji hao kumepokelewa kama changamoto kwa Jose Mourinho kuelekea katika mtanage wa hii leo ambao utakua na umuhimu mkubwa kwa Man Utd.
Man Utd wanatakiwa kushinda mchezo huo ili kujiwe katika mazingira yasiyo na utata ya kusonga mbele kwenye michuano ya Europa League.
Hata hivyo safari ya Man Utd itategemea matokeo ya mchezo mwingine wa kundi lao ambapo Feyenoord ya Uholanzi itakua ikikabiliana na Fenerbahce ya Uturuki.
Endapo Feyenoord watashindwa kuchomoza na ushindi katika mchezo wa hii leo, itakua rahisi kwa Man Utd kusonga mbele hata kama watapoteza mchezo wao dhidi ya Zorya Luhansk.
Michezo mingine ya Europa League itakayochezezwa hii leo.
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI A
Feyenoord v Fenerbahçe
Zorya Luhansk v Manchester United
UEFA EUROPA LEAGUE – GROUP B
Apoel Nicosia v Olympiakos
BSC Young Boys v FC Astana
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI C
Mainz 05 v FK Qabala
RSC Anderlecht v Saint-Étienne
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI D
AZ Alkmaar v Zenit St Petersburg
Maccabi Tel-Aviv v Dundalk
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI E
Astra Giurgiu v Roma
Viktoria Plzen v Austria Vienna
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI F
Sassuolo v KRC Genk
Rapid Vienna v Athletic Bilbao
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI G
Panathinaikos v Celta Vigo
Standard Liege v Ajax
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI H
Konyaspor v KAA Gent
Sporting Braga v Shaktar Donetsk
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI I
FC Red Bull Salzburg v FC Schalke 04
Nice v FK Krasnodar
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI J
FK Qarabag v Fiorentina
PAOK Salonika v Slovan Liberec
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI K
Inter Milan v Sparta Prague
Southampton v Hapoel Be’er Sheva
UEFA EUROPA LEAGUE – KUNDI L
Osmanlispor v FC Zürich
Villarreal v Steaua Bucharest