Mashetani wekundu Man Utd wamepangiwa kukutana na klabu ya Midtjylland ya nchini Denmark, katika hatua ya 32 bora ya michuano ya Europa League.
Man Utd wameangukia kwenye michuano hiyo baada ya kutupwa nje kwenye mshike mshike wa Champions League hatua ya makundi.
Katika droo iliyopangwa muda mchache uliopita, ilitarajiwa huenda Man Utd wangepangiwa kigogo katika michuano hiyo lakini sasa inatazamiwa huenda ikawa ni mteremko kwao, kutokana na uzoefu mkubwa walionao tofauti na Midtjylland.
Kwa upande wa majogoo wa jiji, Liverpool wanaoendeshwa na meneja Jurgen Klopp watakutana na klabu kutoka kutoka nchini Ujerumani Augsburg.
Tottenham Hotspur wao wamepelekwa nchini Italia kupambana na Fiorentina.
Ratiba ya hatua ya 32 bora ya Europa League iliyotokana na droo iliyochezeshwa muda mchache uliopita huko mjini Nyon nchini Uswiz ni kama ifuatavyo.
Valencia v Rapid Vienna
Fiorentina v Tottenham Hotspur
Borussia Dortmund v FC Porto
Fenerbahce v Lokomotiv Moscow
Anderlecht v Olympiakos
Midtjylland v Manchester United
Augsburg v Liverpool
Sparta Prague v Krasnodar
Galatasaray v Lazio
Sion v Braga
Shakhtar Donetsk v Schalke
Marseille v Athletic Bilbao
Sevilla v Molde
Sporting Lisbon v Bayer Leverkusen
Villarreal v Napoli
Saint-Etienne v Basel