Meneja wa klabu ya AS Roma Eusebio Di Francesco amesema kikosi chake kitapaswa kurejea maajabu ya kupindua matokeo dhidi ya Liverpool, kama ilivyokua kwa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona.

AS Roma wapo nyuma mabao matano kwa mawili waliofungwa katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali, ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya wapinzani wao Liverpool juma lililopita.

Di Francesco ametoa kauli hiyo ya hamasa katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali, ambao utachezwa kesho jumatano mjini Roma, Italia.

Mwezi uliopoita AS Roma waliushangaza ulimwengu kwa kupindua matokeo dhidi ya FC Barcelona na kuwaondoka katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, kwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri ambao ulistahili, baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali kwenye uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona, kwa kufungwa mabao 4-1.

“Tunapaswa kuamini tunaweza kurejea maajabu tulioionyesha dunia mwezi uliopita, hakuna linaloshindikana, huu ni mchezo wa soka na lolote linawexza kutokea, tena kwa wakati wowote.” Di Francesco aliwaambia waandishi wa habari.

“Liverpool wana kikosi hatari ambacho kinaweza kukuadhibu wakati wowote, lakini tumeshajitayarisha kuwakabili na tutapambana ili kufikia lengo la kusawazisha mambo ili tufanikishe lengo la kucheza fainali msimu huu na ikiwezekana kutwaa ubingwa.”

AS Roma haijafungwa bao lolote msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya inapocheza katika uwanja wake wa nyumbani, jambo ambalo linaongeza imani kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo.

“Kwa msimu huu tunapokua nyumbani tunapambana vizuri, na ndio maana mpaka sasa hatujaruhusu kufungwa bao hata moja, japo tulipata wakati mgumu tulipocheza dhidi ya Atletico Madrid kwenye hatua ya makundi.” Ameongeza Di Francesco.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 2, 2018
Jurgen Klopp athibitisha kurejea kwa Adam David Lallana