Klabu ya Everton imeibuka na azimio la kutaka kumsajili mlinda mlango wa Man City, Joe Hart baada ya kupata nguvu ya kukamilishwa kwa dili hilo kutoka kwa mwanahisa Farhad Moshiri.

Moshiri ambaye ni mfanyabiashara mkubwa kutoka nchini Iran, ametilia mkazo katika maazimio hayo kwa kuwa tayari kutoa kiasi cha Pauni million 40, kama ada ya uhamisho wa mlinda mlango huyo ambaye inaonekana hayupo kwenye mipango ya meneja mpya wa Man city, Pep Guardiola.

Kutokana na makubaliano hayo, uongozi wa Everton umekubali kwa kauli moja na umesisitiza kuwa tayari kumlipa mshara Joe Hart wa pauni 200,000 kwa juma.

Everton wanasaka mbinu za kumsajili Joe Hart, baada ya kumalizana na mlinda mlango kutoka nchini Marekani Tim Howard ambaye mwishoni mwa msimu uliopita mkataba wake ulifikia kikomo.

Daley Blind: Vyombo Vya Habari Havijamtendea Haki Van Gaal
Alvaro Morata Awachanganya Mashabiki Wa Juventus

Comments

comments