Uongozi wa klabu ya Everton, umeripotiwa kumfuta kazi Roberto Martinez kama meneja wa klabu hiyo.

Taarifa zilizoelezwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports, zimeeleza kwamba uongozi wa The Toffees, umefikia maamuzi ya kutimua kazi meneja huyo baada ya kutopendezwa na matokeo yaliyopatikana katika michezo ya hivi karibuni.

Tangu Machi 5, Everton wamekua hawafanyi vizuri mpaka kufikia usiku wa kuamkia hii leo ambapo walikubali kufungwa mabao matatu kwa sifuru dhidi ya Sunderland.

Martinez anaondoka huku mchezo mmoja wa ligi ya nchini England msimu huu, ukisalia ambapo mwishoni mwa juma hili kikosi cha Everton kitapambana na Norwich City.

Everton kwa sasa wapo katika nafasi ya 12, wakiwa na point 44.

Messi Na Ronaldo Wapambana Kila Mahala
Tottenham Hotspurs Wazima Ndoto Za Man Utd