Kiasi cha pesa kilichotangazwa na uongozi wa klabu ya Everton, kama ada ya usajili wa Romelu Lukaku, huenda kikazikimbiza baadhi la klabu za ligi kuu ya soka nchini England, zilivyoonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo.

Kiasi cha Pauni milioni 65, kimetajwa kama ada ya usajili wa Lukaku ambaye tayari ameshaonyesha dhamira ya kutaka kuondoka Goodison Park, na kwenda mahala pengine kusaka changamoto mpya wa soka lake.

Klabu za ligi ya England ambazo zipo kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji huyo kutoka nchini Ubelgiji ni Chelsea, Arsenal, West Ham United pamoja na Crystal Palace.

Klabu hizo za England zinakabiliwa na upinzani mtizo kutoka Juventus ya Italia pamoja na FC Bayern Munich ya Ujerumani, ambazo zimejiweka vizuri katika harakati za kumuondoa Lukaku huko mjini Liverpool.

Hata hivyo Lukaku, hakuonyesha uwezo wake, wakati wa fainali za Euro 2016 zilizofikia tamati mwishoni mwa juma lililopita kama ilivyokua inatarajiwa, hali ambayo imezua maswali mengi miongoni mwa wadau wa soka duniani kote.

Meneja mpya wa klabu ya Everton, Ronald Koeman naye ameonyesha kuridhika na maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo, ya kutaka kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye anasimamiwa na wakala Mino Raiola.

Msami Afungukia Uhusiano wake na Kajala
Henry Joseph Awaombea Kila La Kheri Walioondoka Mtibwa Sugar