Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imempa adhabu ya kukatwa mshahara wa wiki mbili mshambuliaji wake Wayne Rooney kufuatia kukutwa na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.

Everton inadhamiria kupeleka fedha hizo zinazofikia kiasi cha pauni laki tatu ( £300,000) kwenye kituo cha watu wenye uhitaji maalum.

Pamoja na Rooney mwenye miaka 31 kuomba kusahemewa ili aepuke adhabu hiyo, Everton imebaki na msimamo wake na klabu hiyo itapeleka kiasi hicho cha fedha katika mradi wake wa kusaidia watu wasiojiweza.

Mnamo tarehe 18 mwezi huu Wyne Rooney alikuhumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili baada ya kukamatwa Septemba 1 akiwa anaendesha gari huku amelewa.

Mshambuliaji huyo aliyestaafu kuichezea timu ya taifa ya Uingereza Siku pamoja na hadhabu hiyo atafanya pia kazi za jamii kwa siku mia moja.

 

 

LIVE: Waziri Mkuu akiweka jiwe la msingi mradi wa maji Longido, Arusha
Video: Usione nimekaa kihasara nakula matunda yangu-Nikki wa Pili