Klabu ya Everton imethibitisha kumfungia vilago kocha Sam Allardyce baada ya kocha huyo kuitumikia Everton kwa miezi sita.

Uamuzi wa kumtimua kocha huyo umekuja baada ya mkutano baina yake na mwenyekiti wa klabu hiyo Farhad Moshiri ambaye ameamua kumfungia vilago Allardyce.

Allardyce mwenye umri wa miaka 63 ameiwezesha Everton kumaliza katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu lakini matokeo hayo yameshindwa kulinda kibarua chake.

Kocha huyo atalipwa kiasi kinachokadiriwa kufikia paundi milioni 6 ikiwa ni malipo ya miezi 12 iliyobaki katika mkataba wake.

Kocha wa zamani wa Watford Marco Silva anatajwa kumrithi Sam Allardyce kwani Everton walimtaka tangu mwaka jana mwezi Novemba wakati mreno huyo akiwa Watford.

Kenya yapata mwarobaini wa uhalifu wa mtandaoni
Wachungaji wanusurika kipigo baada ya kushindwa kumfufua mfu

Comments

comments