Watanzania wanaanza mwaka mpya 2017, kwa machungu  baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Madini (EWURA), kutangaza kupandisha bei kwa wastani wa asilimia 8.5, ambapo hata hivyo  nyongeza hiyo ni tofauti na ombi la Shirika la Uzalishaji na usambazaji  wa Umeme(Tanesco).

Bei hiyo mpya itaanza kutumika rasmi Januari 1,2017 imekuja ikiwa ni miezi miwili tu baada ya Tanesco kutuma maombi Ewura ya kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 18 jambo ambalo lilipingwa vikali na wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Felix Ngalamgosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Bodi ya Ewura imefanya uchambuzi kwa makini na kupitia mapendekezo yaliyotolewa na Tanesco na kujiridhisha na hoja hivyo ikafikia uamuzi huo wa kupandisha bei ya umeme.

“Bodi ya Ewura imefanya uchambuzi kwa makini na imeridhishwa na hoja zilizotolewa kuazimia kupandisha umeme kwa asilimia 8.5 badala ya 18.19″amesema Felix.

Aidha, Felix amesema kuwa maeneo ambayo hayatapanda gharama za umeme ni wateja ambao wanatumia umeme chini ya uniti 75 kwa mwezi, hivyo hawatahusika na ongezeko hilo.

 

UFC 207: Amanda Nunes 'amfunza adabu' Ronda Rousey
Video: Meya wa kinondoni azindua mradi wa uboreshaji jiji la Dar es salaam