Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta nchini Tanzania itakoyoanza kutumika leo April Mosi 2020  kwa baadhi ya mikoa.

Ambapo kwa Dar es Salaam bei za rejareja petrol itauzwa sh 2,087, kutoka sh 2,204, dizel sh 1,989, kutoka sh 2, 153, na mafuta ya taa yatauzwa sh 1, 993, kutoka sh 2,116, huku bei za jumla EWURA imesema petrol sh 116, dizel sh 164 na mafuta ya taa 192.

EWURA imesema mabadiliko hayo yanatokana mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji.

Kadhalika bei imeshuka katika mikoa ya kaskazini Tanga, Kilimanjaro, Arusha, na Manyara bei zimeshuka kwa petroli sh 86, dizel sh 86, na mafuta ya 85.

Hata hivyo mikoa ya kusini Mtwara, Lindi na ruvuma bei itakayo tumika ni ya mwezi machi kwa kuwa hakuna mafuta yaliyopelekwa katika bandari ya Mtwara.

Aidha mamlaka hiyo imesisitiza wananchi kutumia simu za mkononi kujua bei yamafuta eneo husika walilopo kupiga *152*00# na kufuata maelekezo.

 

Hamdoun apewa programu maalum Azam FC
Hizi hapa nafasi 10 za ajira Tanzania Mwezi April

Comments

comments