Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Modestus Lumato, ametangaza kupungua kwa bei a rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa ambapo bei hizo zitaanza kutumika kuanzia leo.

Februari mwaka huu bei za rejareja za mafuta ya dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimeshuka kwa shilingi 190 kwa lita na shilingi 142 kwa lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 4 Januari mwaka huu na bei ya rejareja ya mafuta ya petroli haibadiliki.

Lumato amesema, kwa mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara), bei za rejareja mwezi huu kwa mafuta ya petroli na dizeli zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa katika toleo la Januari 4, mwaka huu.

Aidha, ameomngeza kuwa kwa mikoa ya Kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma), bei za rejareja za mwezi huu kwa mafuta ya petroli na dizeli zimeshuka kwa shilingi 118/lita na shilingi 160 kwa lita, mtawalia, ikilinganishwa na toleo la tarehe 4 Januari mwaka huu.

Asilimia 50 ya Dawa Afrika ni bandia
Serikali yatoa wiki mbili kwa SUMA JKT, NHC