Serikali ya Wilaya ya Ilala imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za kuwepo zoezi la uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa watumishi wa umma katika wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema

Akizungumza na Dar24 kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa zoezi hilo linafanyika kwa lengo la kufanya mapitio na kuweka sawa taarifa zote za watumishi kwenye mfumo na sio vinginevyo.

“Lengo ni kupitia upya na ku-update database ya taarifa za wafanyakazi wote na sio vinginevyo. Sio kwamba ni uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa lengo tofauti la uhakiki kama linavyotafsiriwa vinginevyo,” Mjema aliiambia Dar24.

Juzi, gazeti la Tanzania Daima lilimkariri mkuu wa shule moja katika wilaya ya Ilala ambaye hakutaka jina lake litajwe akieleza kuwa wametakiwa kuwasilisha vyeti vyao ikiwa ni pamoja na vyeti vya ndoa kwa lengo la kufanyiwa uhakiki.

Zoezi la uhakiki wa vyeti vyote kwa watumishi wa umma lilitangazwa nchi nzima kupitia Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, lengo likiwa kuhakiki na kuweka sawa taarifa zote za watumishi. Zoeizi hilo la uhakiki linaloendelea limepelekea kubainika kwa maelfu ya watumishi hewa.

 

Mtifuano Wa Ulaya Washika Kasi, Real Madrid Wabanwa
Live: Maswali na majibu kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma