Vanessa Mdee ambaye ameshakumbwa na changamoto kubwa kwenye safari yake ya muziki na maisha ya kawaida, ameweka wazi njia anayotumia kuzika nyakati ngumu za matatizo yaliyomkumba.

Vee Money ambaye alitembelea ofisi za Dar24 hivi karibuni, alifunguka kwenye mahojiano maalum na tovuti hiyo kuwa ameshakutana na misukusuko mingi kwenye maisha yake, nyakati zilizoupasua moyo wake na kutaka kumkatisha tamaa lakini siku zote hujitahidi kutojenga kibanda cha kumbukumbu za nyakati hizo.

“Kama ulivyosema kwenye maisha kuna ups and downs… the moment you can feel heart broken and discouraged. Lakini mimi najitahidi nisidwell kwenye hizo moments,” Vee Money aliiambia Dar24.

“Yaani chochote kiende [kombo] nasema, you know what ‘Inshallah’, Mungu ndiye anayejua. God is in control for me. Kwa sababu nimeshakutakana na nyakati ngumu lakini hata sikumbukagi kwa sababu siwekagi akiba ya vitu vibaya, najaribu kuweka kumbukumbu ya vitu vizuri zaidi kuujaza moyo wangu na faraja” aliongeza.

Mwimbaji huyo wa ‘Kisela’ ambaye bado anatibu maumivu ya kuachana na mpenzi wake, Juma Jux huku akieleza wazi kuwa bado anampenda, ameeleza misukosuko aliyowahi kuipitia kwenye safari yake ya muziki, wasanii wa kike waliomvutia kuingia kwenye muziki hapa Tanzania, Siri ya kupata michongo ya kufanya matangazo ya bidhaa kubwa na mengine mengi.

Angalia video hii kupata kwa undani maelezo ya Vee Money, subscribe kupata mahojiano ‘exclusive’ ya wasanii unaowakubali zaidi.

Magazeti ya Tanzania leo Julai 25, 2017
Video: Chama cha ADC chamuomba JPM kulegeza masharti ya siasa