Mtendaji na msemaji mkuu Idara ya Uhamiji, Ally Mtanda ametoa ufafanuzi wa kina juu ya mambo muhimu ya kuzingatia kwa mtu anayetaka kushughulikia hati ya kusafiria maarufu kama pasipoti.

Mtanda amesema kwa muombaji wa hati hiyo ni muhimu kuzingatia taratibu zote kwa mujibu wa sheria ambazo zinamtaka mtu huyo kumiliki hati.

Aidha ametoa onyo kali kwa wale ambao si raia wa Tanzania kughushi nyaraka ili waweze kupatiwa hati hiyo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao.

Pia ametoa ufafanuzi juu ya taratibu nzima za kubadilisha hati ya zamani kuwa hati ya kielektroniki. Kusikiliza zaidi  bonyeza link hapo chini.

Jorge Sampaoli akataa 'kutii amri', kulipwa fidia
Juan Cuadrado akubali yaishe kwa Ronaldo

Comments

comments