Wakati ‘Sinaga Swaga’ ikiendelea kutikisa mitaa na vyombo mbalimbali vya habari kutokana na utata wa mashairi ya majigambo yanayowakwaruza baadhi ya rapaz nchini, Rapa Young Killer ameandaa kombora jingine kushindilia alipoishia.

Akizungumza katika mahojiano maaluma na Dar24 iliyomtembelea mtaani kwake jana, Young Killer amesema kuwa wiki ijayo ataachia audio na video mpya za remix ya wimbo wake ‘Sinaga Swaga’, kumalizia pale alipoishia.

Alisema ameamua kufanya remix ya wimbo huo unaofanya vizuri hivi sasa kutokana na kile kinachoendelea kuzungumzwa kuhusu kila mstari wa wimbo huo.

“Hii ni exclusive, sijawahi kuisema kokote naisemea hapa Dar24… wiki ijayo mashabiki wangu wajiandae naachia ‘Sinaga Swaga Remix’, itakuwa na audio na video. Kila kitu kiko tayari………,” Killer alifunguka kwenya mic ya Dar24.

Akizungumzia uhusiano wake wa sasa na waliowataja kwenye ‘sinaga swaga’, ikiwa ni pamoja na rapa Young Dee na Dogo Janja, Msodoki alieleza kuwa hajawahi kuwa na ushikaji wa karibu na marapa hao zaidi ya kazi. Kwahiyo kinachoendelea kufanyika ni kazi tu iliyoweka ushikaji kando.

Rapa huyo ambaye ni CEO wa Matunzo Zero Unit Entertainment ameeleza kuwa wimbo huo ambao alianza kuurekodi kama masihara ambayo yaligeuka kuwa hit, umefanya vizuri kwakuwa yeye huwa ni ‘hit maker’ asishindwa kupika muziki mzuri kila siku.

“Sijawahi kufanya wimbo mbaya na sitakuja kufanya wimbo mbaya. Wimbo unaweza usipewe nafasi tu kwenye vyombo vya habari lakini mimi siwezi kufanya wimbo mbaya,” alisema Msodoki.

Kaseja Mchezaji Bora Wa Januari Ligi Kuu Tanzania bara
Leonardo Bonucci Kukaa Jukwaani