Hatua ya washambuliaji wa Young Africans kushindwa kutumia vizuri nafasi zinazotengenezwa, imetajwa kama tatizo kubwa linaisumbua timu hiyo msimu huu 2019/20.

Kocha mkuu wa Young Africans, Luc Eymael amesema amekuwa akiwapa mazoezi wachezaji wake ya kutumia mipira ya krosi katika ufungaji, lakini washambuliaji wake hawafanyi hivyo wanapokua kwenye majukumu ya michezo ya mashindano kama Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji ameweka wazi mapungufu hayo, baada ya kikosi chake kushindwa kufurukuta mbele ya Namungo FC juzi Jumanato kwenye mchezo wa mzunguuko wa 31 wa Ligi Kuu, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

“Klop na Guadiola unawaona wakiingia uwanjani? Nimewafundisha na wanajua nini wanachotakiwa kufanya lakini sio mimi kwenda tena kufunga, nafasi nyingi tunatengeza siku hizi lakini hatufungi,” alisema.

Akizungumzia mchezo dhidi ya Namungo FC, kocha Eymael amesema anawapongeza wachezaji wake kwa kujituma mwanzo mpaka mwisho wa mchezi na kusawazisha.

“Ilibidi niingize viungo na washambuliaji ili kuweza kupata goli na tulifanikiwa, wengi wananiona kama vile sina akili lakini mimi sijahusika katika usajili,” alisema.

Young Africans inaendelea kusalia katika nafasi ya tatu ikiwa na alama 57 huku Namungo ikiwa nafasi ya nne na alama 55, kesho klabu hiyo ya Jangwania itacheza mchezo wa mzunguuko wa 32 kwa kuikabili Ndanda FC kutoka Mtwara.

TPLB: Tutakabidhi ubingwa VPL kwa utaratibu
Uchaguzi Malawi: Upinzani waongoza matokeo ya awali