Chama cha soka nchini England FA, huenda kikamfungulia mashtaka ya kinidhamu meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho baada ya kubainika kulikua na mawasialiano kati yake na meneja msaidizi, Steve Holland sambamba na Rui Faria.

Mourinho alifanya hivyo, kutokana na adhabu ya kufungiwa kuingia uwanjani katika mchezo dhidi ya Stoke City, kufuatia utovu wa nidhamu ambao aliuonyesha mara baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Southampton kwa kumsemea mbovu muamuzi mbele ya waandishi wa habari.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwepo kwa kifaa cha mawasilino kwenye benchi la ufundi la Chelsea na mara kadhaa meneja msaidizi Steve Holland alionekana akizungumza na kwa kijificha.

Hata hivyo uchunguzi bado unaendelea kufanya na ikibainika kuliwepo na mchezo huo ambao haukutakiwa kuwepo, Mourinho ataadhibiwa zaidi kutokana na kanuni za kinidhamu ambazo zipo chini ya chama cha soka nchini England FA.

Jambo lingine ambalo huenda likaiingiaa klabu ya Chelsea kwenye hatari ya kuadhibiwa na FA, ni hatua ya mameja wasaidizi kushindwa kufika kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Katika mchezo huo Chelsea walikubali kufungwa bao moja kwa sifuri.

Lowassa Amuuliza Maswali Haya Rais Magufuli
Viti Maalum Vyapelekea Viongozi Wa Chadema Kujiuzulu