Maamuzi ya ukakasi wa utoaji wa Penati yamefanya wasimamizi wa mfumo wa marefa wasaidizi (VAR) kukosolewa vya kutosha nchini England.

Makosa hayo yalitokea kwenye michezo tofauti Jana Alkhamis baada ya Manchester United kunufaika na tuta ambalo Bruno Fernandes alijiangusha na kumlanghai mwamuzi, Ward wa Southmpton aliongopa kuwa ameangushwa katika kipute dhidi ya Everton.

Kufuatia makosa hayo Chama cha Soka England (FA) kimeomba radhi kwa kushindwa kutoa maamuzi sahihi kwa kuwa mfumo wa (VAR) haukufanya kazi vizuri, kwani uliamuru Penati pasipo Penati penye Penati ukikataa.

Bruno Fernandes alidai kukanyagwa katika ushindi wa Manchester United wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Aston Villa.

James Ward-Prowse alipiga shuti iliyogonga mwamba baada ya kupewa Penati yenye utata wakati Southampton ilitoka ya kufunganabao moja kwa moja dhidi ya Everton.

Klabu ya Tottenham ilitakiwa kupewa tuta baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Harry Kane kuangushwa kwenye eneo la hatari kwa kusukumwa na Joshua King na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana, lakini mwamuzi akapeta kwa madai alijiangusha makusudi.

EPL imethibitisha kuwa Manchester United na Southampton hazikustahili kupewa matuta kwenye michezo ya katikati ya juma hili lakini Tottenham walitakiwa kupewa penati kwa kuwa zilikuwa za wazi.

Mchezaji wa zamani wa Everton Tim Cahill, alisema “Pindi mchezaji anapojaribu kumuongopea mwamuzi kutoa penati lazima refarii awe karibu kuangalia uwezekano wa kuona tukio vyema.”

Shirikisho la Soka duniani FIFA linachukua jukumu la moja kwa moja la kutoka kwa Bodi inayotunga sheria za kandanda IFAB na linatarajiwa kusisitiza uwepo wa muendelezo wa matumizi mazuri ya VAR katika zaidi ya ligi 100 za kimataifa kwa masuala kama vile matumizi ya skrini au televisheni za pembeni ya uwanja.

Tetesi za usajili: Leicester City kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid
Bernard Morrison apaza sauti kwa mashabiki

Comments

comments