Chama cha soka nchini England FA, kimetoa taarifa za kuendelea kumuunga mkono rais wa UEFA, Michel Platini, licha ya kufungiwa kwa siku 90, kutokana na tuhuma za ufusadi zinazomuandama ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA.

FA, wametangaza msimamo huo, saa chache baada ya FIFA kuweka hadharani adhabu kwa viongozi ambao wanatuhumiwa kujihusisha na kosa la ufisadi na watafanyiwa uchunguzi na serikali ya nchini Uswiz.

Taarifa iliyotolewa na FA, imeeleza kwamba, viongozi wa chama cha soka nchini England, wataendelea kumuunga mkono na kumuheshimu Platini kama rais wa UEFA, mpaka itakapothibitika kama alijihusika na tuhuma zinazomkabili kwa sasa.

Juma lililopita, viongozi wa ngazi ya juu wa FA, walikutana na kufikia maamuzi ya kumuunga mkono ama kuachana na Platini, lakini maazimio ya walio wengi yaliegemea upande wa kuwa na imani na kiongozi huyo ambaye alishatangaza nia ya kuwania kiti cha urais wa FIFA.

Paltini, walifikishwa mbele ya kamati ya maadili na kujadiliwa kwa kina na imeamuriwa ni bora wakakaa pembeni, ili kupisha uchungzi wa tuhuma zilizoibuliwa na serikali ya nchini Usiwz chini ya mwanasheria mkuu wa nchi hiyo.

Liverpool Wamalizana Na Jurgen Klopp
Mbeya City Wachimba Mkwara