Klabu za Chelsea na Tottenham Hotspur zimekutwa na hatia na kutozwa faini ya Pauni 375,000 na 225,000 kufuatia utovu wa nidhamu uliojitokeza wakati wa wakali hao wa jijini London, walipokutana mwanzoni mwa mwezi huu (Mei 2) kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Chama cha soka nchini England, FA kimejiridhisha kwa kusikiliza utetezi uliowasilishwa na klabu hizo, na kimebaini kulikua na mapungufu ya utovu wa nidhamu kwa wachezaji wa timu zote mbili.

Taarifa iliyotolewa na FA imeeleza kwamba klabu hizo zilikiuka na kuvunja kanuni na ligi kuu ya soka nchini England kifungu cha E20, ambacho kinatoa mamlaka kwa mabenchi ya ufundi kusimamia na kuzuia jazba ambazo zinaweza kujitokeza miongoni mwa wachezaji wakati mchezo ukiendelea.

Wachezaji wa Chelsea na Spurs wakiwa katika malumbano yaliyotokana na moja ya matukio ya utovu wa nidhamu uliojitokeza wakati wa mchezo wao wa Mei mbili.

Katika mchezo huo, matumaini ya Spurs kuendelea kuwa katika mbio za ubingwa wa nchini England, ndipo yaliyeyuka na kuwaacha Leicester City akitawazwa kuwa mabingwa, kufuatia matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili.

Roy Hodgson Kutembelea Nyota Ya Leicester City Euro 2016
Maduka, Magari yanayowakataa wana CCM yafungiwa, Maalim Seif Asema neno