Chama cha soka nchini England (FA) kimemfungulia mashtaka meneja wa klabu ya Stoke City Mark Hughes, kufuatia utiovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa mchezo wa ligi kuu uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Tottenham.

Katika mchezo huo ambao ulishuhudia Stoke City wakikubali kuchabangwa mabao manne kwa sifuri, Hughes alitakiwa kuondoka katika benchi la ufundi la Stoke City na mwamuzi Anthony Taylor, kifuatia maneno makali anayodaiwa kuyatoa mbele ya mwamuzi namba nne, mara baada ya kikosi chake kufungwa bao la pili.

Mbali na kutoa maneno makali kwa mwamuzi huyo, Hughes pia anatuhumiwa kuvuka eneo lake la kutoa maelekezo kwa wachezaji, japo alipewa onyo zaidi ya mara mbili.

Hughes ametakia kuwasilisha utetezi wa tuhuma zinazomkabili kabla ya kuzama kwa jua siku ya ijumaa.

Stoke City kwa sasa inaburuza mkia wa msimamo wa ligi ya nchini England (PL), ikiwa imejikusanyia point moja tangu msimu wa 2016/17 ulipoanza kati kati ya mwezi uliopita.

Mchezo dhidi ya Middlesbrough uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja, ndio unaipa klabu hiyo ya Britannia Stadium point moja.

David Ospina Amkuna Arsene Wenger
Ripoti Yatolewa Ufaransa na Uingereza Zilichangia kumng'oa Gaddafi Libya