Kocha mashuhuri barani Ulaya Fabio Capello, amesema alikataa kazi ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya Italia mara baada ya kuondoka kwa Antonio Conte mwezi Julai mwaka huu.

Capello, ambaye aliwahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England na urusi, amesema wakati wa mchakato wa kumsaka mkuu wa benchi la ufundi la The Azzurri alipata taarifa kadhaa za ushawishi lakini alikataa kata kata.

Capello mwenye umri miaka 70, amesema sababu kubwa ya kukataa wito wa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia, ni kutokua tayari kufanya kazi na viongozi wa chama cha soka nchini humo.

Hata hivyo kocha huyo hakuweka wazi undani wa sababu zinazomzuia kufanya kazi na viongozi wa chama cha soka nchini Italia.

“Nilizungumza na baadhi ya wadau wa soka nchini Italia na walinitaka kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, ila nilikataa kutokana na dhamira yangu ya kutokua tayari kufanya kazi na viongozi wa chama cha soka.”

“Inatosha kusema nilikataa kazi ya kuwa kocha mkuu wa Italia, mambo mengine yatabaki kuwa moyoni mwangu, jambo kubwa ninapenda kumtakia kila la kheri kocha wa sasa wa The Azzurri Giampiero Ventura,” Alisema Capello.

“Kuhusu mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Liechtenstein, watu wengi wanaamini Italia huenda ikaibuka na ushindi kirahisi, lakini kwangu  naamini mambo yatakua magumu.”

Claudio Bravo Achafua Hali Ya Hewa Etihad Stadium
Video: Kampuni ya DataVision International kuongeza ufanisi katika sekta za kifedha