Kiungo kutoka nchini Hispania na klabu ya AS Monaco ya Ufaransa Francesc “Cesc” Fàbregas Soler ametangaza rasmi kustafu soka la ushindani.

Fabregas alijiunga na AS Monaco January 2019, ambapo aliichezea klabu hiyo katika michezo 68 na kuisaidia kunusurika kushuka daraja msimu uliopita, na msimu huu amekua mmoja wa wachezaji walioifikisha katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi ya Ufaransa nyuma ya PSG na Marseille

“Kwanza, Nilikuwa bado nahitaji kucheza, sikuhitaji kumaliza Kama hivi. Ulikuwa ni msimu mbaya sana kwangu. Nahitaji kuwa na furaha,na kumaliza vizuri.”

“Nilikuwa tayari kwa kilakitu. Ilikuwa ni klabu ndogo katika mashindano makubwa na ilikuwa na uwezakano wa kushuka daraja ila kila kitu kimeenda sawa. Niliamua kwenda kwenye klabu ambayo nitapata nafasi ya kucheza na wananiamini ( AS Monaco)”

“Nilisaini mkataba na club hii kwa lengo moja tu nalo ni kuisaidia isishuke daraja ambapo ilikuwa nafasi ya 19 ikiwa na alama 13. Nilichukua maamuzi magumu sana kwani kushuka daraja ilikuwa na jambo linalowezekana lakini tuliweza isaidia timu na ikamaliza ktk nafasi nzuri. Nafurahi sana kuifanya timu isishuke daraja.”

“Nilipokuja hapa Thieny Henry na Makamu wa Raais waliniambia niwasaidie vijana kukua. Hii ndo lilikuwa Jambo muhimu zaidi.”

“Lakini leo najisikia mwenye upendo na amani kwa kile nilichofanya kwa vijana hawa. Natumai tumesaidiana sana. Sitoacha kuwafuata na kuzungumza nao.”

“Kwangu hii misimu miwili ilikuwa ya muhimu sana. Japokuwa huu msimu wa mwisho ulikuwa ni msimu wangu mbaya kuwahi kutokea katika maisha yangu. Na nimejifunza vingi Sana” amesema kiungo huyo wa zamani wa klabu za Arsenal, Chelsea na FC Barcelona.

Cesc atakumbukwa kwa pasi nzuri za mwisho katika timu ya Taifa ya Hispania na Klabu zote alizozitumikia.

Hassan Shehata amchana Mo Salah
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 22, 2022