Utajiri wa mmiliki wa Kampuni ya Facebook, Mark Zuckerberg umeporomoka kwa zaidi ya $6 bilioni ndani ya saa chache, baada ya mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp kupotea hewani Jumatatu.

Kwa mujibu wa Bloomber, utajiri wake binafsi umeporomoka na sasa ana utajiri wa $121.6 bilioni, ambao unamuweka kwenye nafasi ya tano ya watu matajiri zaidi duniani, kutoka nafasi ya tatu aliyokuwa anaishikiliwa saa chache kabla ya tatizo hilo lililoikumba Facebook.

Forbes wameandika kuwa Mark Zuckerberg amepoteza $5.9 bilioni ikitaja chanzo kikuu kuwa ni kuporomoka kwa bei/thamani ya hisa za kampuni ya Facebook.

Imeeleza kuwa tangu taarifa hizo zilipoifikia dunia, thamani ya hisa za Facebook iliporomoka kwa 5% Jumatatu pekee. Hatua hiyo inaongezea katika poromoko la 15% la tangu Septemba mwaka huu.

Bundi mbaya ameendelea kulia juu ya fedha za Zuckerberg, ambapo imeelezwa kuwa tangu Septemba 2021 ameshapoteza kiasi cha $19 bilioni katika sehemu ya utajiri wake.

Habari kubwa kwenyemagazeti leo, Oktoba 5, 2021
Facebook, WhatsApp, Instagram zatoweka 'duniani', nini chanzo?