Kampuni ya Facebook hivi karibuni ilimkatalia mwanasiasa wa Denmark ambaye ni mbunge wa chama cha Social Democratic, Mette Gjerskov kupakia picha ya sanamu ya nguva kwa madai kuwa ilikuwa inakinzana na sera ya mtandao huo.

Gjerskov alieleza kuwa alipokuwa akijaribu kupakia picha ya sanamu  ya nguva alipokea ujumbe unaomzuia kufanya hivyo kwa madai kuwa picha hiyo ilikuwa ikionesha sehemu ya’ utupu’ au maudhui ya mapenzi.

Alifahamishwa kuwa picha hiyo ni kinyume cha sera ya Facebook inayozuia kuchapishwa kwa picha zenye maudhui ya kimapenzi au zinazoonesha ‘utupu’.

Hata hivyo, alieleza kuwa baada ya muda Facebook ililegeza msimamo wake na kumruhusu kuipakia picha hiyo. Picha hiyo ya sanamu ya nguva iliyotengenezwa kwa shaba inapatikana mjini Copenhagen.

Septemba mwaka jana, Facebook ilikataa kampuni moja ya kitalii kupakia picha ya mwanamke akiwa amesimama ‘mtupu’ mbele ya vioo. Lakini baadaye iliiruhusu picha hiyo na kueleza kuwa ilikuwa imezuiwa kimakosa.

Chanzo: BBC

 

Yaliyojili leo Mahakama Kuu, Kesi ya Lembeli Kupinga Ubunge wa Kishimba
JKT Ruvu Wawavutia Kasi Maafande Wenzao