Kampuni ya Facebook imeondoa matangazo ya kampeni ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutokana na kutumia alama ya pembe tatu nyekundu, inayofanana na ile iliyotumika na utawala wa ‘Nazi’ wa Ujerumani.

Facebook imedai matangazo hayo yaliyokuwa kwenye kurasa za Rais Trump pamoja na Makamu wake, Mike Pence na kuondolewa baada ya saa 24, yalienda kinyume na Sera yake ya chuki na hawaruhusu alama zozote zinazochochea chuki.

Timu ya kampeni ya Trump imesema tangazo hilo lilikuwa linalenga kundi la maandamano la Antifa ambalo linadaiwa kutumia alama hiyo.

Hivi karibuni, Rais Trump alituhumu kundi hilo kuhusika kuanzisha maandamano ya vurugu nchini Marekani kufuatia kifo cha Georgr Floyd aliyefariki mikononi mwa Polisi Mei 25 mwaka huu.

TAKUKURU yamnasa Salum Mkemi
Vanessa Mdee atangaza kuacha muziki, 'Umejaa mabaya mengi'