Wamiliki wa mtandao wa Facebook wanakabiliwa na kitanzi cha faini ya dola za kimarekani bilioni 22 ($22 billion) kwa kufanya udanganyi wakati wa kuununua mtandao wa WhatsApp.

Umoja wa Ulaya umetoa adhabu hiyo kwa kampuni ya Facebook kwa madai kuwa iliwasilisha taarifa za uongo kwa Tume ya Umoja wa Ulaya ili kupata kibali cha kufanya biashara hiyo, Oktoba 2014.

“Tume ya Umoja wa Ulaya imewatumia Facebook tamko la pingamizi ikituhumu kampuni hiyo kwa kuwasilisha taarifa zisizo sahihi mbele ya Tume wakati wa kufanyiwa uchunguzi kuhusu manunuzi ya WhatsApp,” imeeleza taarifa ya Umoja wa Ulaya.

Facebook imedaiwa kuwa wakati wa kuwasilisha taarifa yake ya kufanya manunuzi hayo Oktoba mwaka 2014 ilieleza kuwa hakuna namna ambayo inawezekana Facebook na WhatsApp zikaunganishwa, lakini mwezi Agosti mwaka huu, mtandao wa WhatsApp ulisema kuwa utaanza ku-share data na Facebook.

Taarifa ya WhatsApp iliibua hisia kwa Umoja wa Ulaya kwamba Facebook ilidanganya kwa makusudi au ilifanya uzembe wakati wa kuwasilisha taarifa yake kwa Tume hiyo.

Facebook imepewa hadi Januari 31 mwakani kujibu madai ya Umoja wa Ulaya dhidhi yake.

Hata hivyo, msemaji wa Facebook amesema kwamba wanaheshimu kazi ya Tume hiyo na kwamba wanaamini mapitio mengine yataonesha wazi kwamba mtandao huo ulitoa taarifa hiyo kwa nia njema na sio kwa lengo la kufanya udanganyifu.

Chanzo: AFP

Nay wa Mitego achukua hatua kumsaidia Chid Benz kuachana na ‘Unga’
Video: Kijana aliyeishi maisha ya ajabu, 'nilitengeneza Mamba...'