Mtandao wa Facebook umeanzisha toleo jipya kwa ajili ya watoto wenye umri wa kati ya miaka 6 hadi 12.

Kupitia toleo hilo, watoto wataweza kuchat kwenye Facebook wakiwa chini ya uangalizi wa wazazi. ‘Messenger Kid’ itaanza kutumika nchini Marekani kwa majaribio, ikianza na watumiaji wanaotumia simu za Apple (iOS).

“Kuna ulazima wa kuwa na App inayowapa watoto nafasi ya kujiunga na dunia ya watu wanaowapenda, kutuma picha na video lakini wakiwa chini ya uangalizi wa wazazi,” amesema Meneja wa Bidhaa wa Facebook, Loren Cheng.

Amesema kuwa mtandao huo umeanzisha App hiyo maalum kwani watoto wamekuwa wakijiunga na Facebook wakitoa maelezo ya uongo, hivyo kutokuwa chini ya uangalizi wa wazazi.

Wamesema kuwa utafiti umewaonesha kuwa asilimia 93 ya watoto wenye umri kati ya miaka 6 hadi 12 nchini Marekani huwa na ‘Tablets’ au simu za kupapasa (Smartphone).

Video: Mbunge amwaga mboga CUF, ataja sababu za kujiuzulu
Ubinafsi ndani ya CCM umetukosesha majimbo- Kalogeresi