Afrika ni moja ya bara lililobarikiwa kuwa na makabila mengi yenye mila na desturi tofauti tofauti.

Leo nitakufahamisha kuhusu makabila ya watu toka Kaskazini mwa Namibia yajulikanayo  kama Ovahimba na Ovazimba wanaoishi katika mkoa wa Kunene na Omusati.

Watu wa kabila hilo sio wengi kwa ujumla wao wanafikia 50,000 ambapo wanawake hujishughulisha na majukumu  ya nyumbani  pamoja na ufugaji ng’ombe huku waume zao wakiwa wanajishughulisha na uwindaji.

Utajiri wa watu kutoka makabila haya hutambulika kwa umiliki wa  idadi kubwa ya ng’ombe .

Watu wa  makabila haya wana namna tofauti ya kumpa heshima mgeni mara tu awatembeleapo nyumbani kwao.

Mgeni wa kiume akitembelea familia yeyote basi kwa heshima na adabu mke wa baba mwenye nyumba hutakiwa kulala na mgeni huyo na kushiriki nae tendo la ndoa.

Kwa utaratibu huo baba mwenye nyumba humpa heshima hiyo mgeni na kumpisha chumba anacholala yeye na mke wake kwa usiku huo na kumwachia mgeni alale na mke wake na yeye kulala chumba kingine.

Iwapo nyumba hiyo ikawa haina chumba cha ziada cha kulala basi baba mwenye nyumba itampasa alale nje ya nyumba yake.

Vivyo hivyo endepo marafiki wa mke wa mwenye nyumba ikatokea wamekuja kumtembelea rafiki yao basi mke nae hana budi kumwachia mume wake ashiriki tendo la ndoa na rafiki zake hao, kwa mujibu wa mila na desturi hizo hili hutokea kwa nadra sana.

Utaratibu wa mila hizo una faida kubwa kwa mujibu wa wahusika ambapo wanesema kwa kufanya hivyo inapunguza wivu wa mapenzi na kudumisha mahusiano, na kwa makabila haya mwanamke hana sauti kwa mume wake.

Orodha ya wenyekiti na makamu wenyekiti kamati ya kudumu ya bunge 2018-2020
Video: Spika ang'oa vigogo, Kauli nne tata mwanafunzi UDSM 'aliyetoweka'