Mchungaji mstaafu Richard Jackson Hananja amesema kuwa wanawake ni viumbe wa tofauti ukilinganisha na mwanaume, ni viumbe wanaoishi kwa hisia wanaanza kuhisi ndipo wanafikiri ukilinganisha na mwanaume anafikiri alafu anatenda.

Mchungaji mstaafu Richard ameyasema hayo wakati akijibu swali la mtangazaji wa Dar24Media kupitia kipindi cha mahojiano la kwanini wanawake wengi wanaoneka kwenda kanisani kwa wingi.

Amesema kuwa kutokana na hali ya kuanza kuhisi ukitangaza jambo lolote wanawake hujitokeza kwa wingi wakidhani kuna sauti ya matumaini katika jambo waliloliendea.

Mwananmke anaweza akaamka asubuhi akaanza kuhisi hunipendi ndugu zako pia hawanipendi,” Amesema Mchingaji mstaafu Richard.

Ameongeza kuwa wanawake hawapenda iufumbuzi wa jambo bali wanachotakiwa kupata ni faraja.

Ahadi yatimia soko la Makangarawe Temeke
Trump kuja na mtandao wake wa kijamii