Gavana wa jimbo la Alabama nchini Marekani, Robert Bentley amekumbwa na kashfa ya kutumia vibaya madaraka yake kuituma nyumbani kwake helikopta ya Jeshi la Polisi kumfuatia pochi aliyoisahau.

Robert Bentley

Robert Bentley

Taarifa za kiuchunguzi zilizotolewa hivi karibuni zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea mwaka 2014 na safari hiyo ya kufuata pochi ya Gavana huyo iligharimu $4,000 (zaidi ya shilingi milioni 8).

Uchunguzi huo umebainisha kuwa Gavana huyo aliondoka Tuscaloosa kuelekea kwenye nyumba yake iliyoko ufukweni, umbali wa safari ya saa tano kwa gari lakini alisahau pochi yake kwa bahati mbaya, ndipo alipoamuru ifuatwe.

Maafisa wa Jeshi la Polisi walitumia helikopta ya Jeshi hilo kutekeleza agizo la Gavana huyo kwa haraka na kwa ufanisi.

Hata hivyo, Bentley ambaye anakabiliwa na shiniko la kujiuzulu kutokana na kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono amepinga kuhusika na kashfa ya kuituma helikopita akidai kuwa aliwaagiza wafuate pochi lakini hakuwaagiza kutumia helikopita.

“Sikuwaambia watumie helikopta. Mimi ni Gavana, ni lazima uwe na pochi yako kwa sababu za kiusalama. Na ni lazima niwe na pesa. Ni lazima ningenunua kitu cha kula. Na nilihitaji vitambulisho vyangu,” aliuambia mtandao wa AL.com

Ripoti: Walio-‘like’ coment ya aliyetoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli wasakwa na Polisi
Serikali kuifumua Dar na kuipanga upya