Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na dhoruba mbalimbali za mambo ya hali ya hewa kama kimbunga ili wananchi wawe na ufahamu wa elimu lakini pia kuwa na utayari endapo majanga kama vimbunga yakitoa.

Akizungumza katika kipindi cha mahojiano na Dar24Media kuhusu tabia za kimbunga, Meneja kituo kikuu cha utabiri TMA Samwel Mbuya, amesema kuwa kimbunga kina tabia ya kusafiri kwa kasi tofauti kutoka eneo moja kwenda eneo lingine.

Aidha amesema kuwa kadiri mazingira yanavyobadilika na kimbunga hubadilika.

“Kadiri kinavyokutana na mazingira rafiki kinaweza kuongeza nguvu, mwendo, mzunguko wake ukaongezeka kinapokutana na mazingira kinzani kinaweza kikapungua nguvu na pia hata kupunguza mwendo kinapokutana na vikwazo ambavyo ni mifumo mingine ya hali ya hewa,” amesema Mbuya.

Ameongeza kuwa kimbunga kina tabia ya kuambatana na dhoruba ya upepo pamoja na mvua nyingi.

Infinix yanyakua tuzo ya nidhamu duniani 2021
Zebaki inavyoathiri maisha ya wachimbaji Tanzania