Ugonjwa wa Ebola ni ugonjwa wa hatari na wa mlipuko unaosababishwa na Virusi viitwavyo Ebola, unaambukiza haraka binadamu na wanyama mwitu (hayawani) kama kima, sokwe, popo, ndege, mijusi, amfibia, na kadhalika.

Japokuwa hakuna mazingira maalum ambamo virusi vya Ebola vinapatikana, lakini wataalamu wanasema virusi hivyo vinapatikana kwa mnyama ambaye anapatikana zaidi barani Afrika.

Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola umetokea katika nchi nyingi na bado unaendelea kupukutisha maisha ya watu wengi hasa barani Afrika.Barani Afrika nchi ambazo zimethibitika kuzurika na Evola ni pamoja na nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea, Ghana, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Gabon, Sudan, Ivory Coast, Uganda na kadhalika.

Ugonjwa wa Ebola unaweza kusambazwa kwa njia mbalimbali kama ifuatavyo.

Kugusana moja kwa moja na mtu ama mnyama mwenye ugonjwa huo, Kugusana moja kwa moja na damu ama majimaji (mate au mafua) ya mtu mwenye ugonjwa huo katika familia, Kugusa vifaa vya tiba vilivyo na virusi vya ugonjwa huo kama sindano, Kutumia vifaa visivyochemshwa katika hospitali kama sinano, Kula ama kushika vinyesi vya wanyama wenye ugonjwa huo, Kuvuta hewa yenye virusi vya ugonjwa huo katika mazingira ya hospitali na Kutumia nyama ya wanyama walioathirika kama kitoweo.

Mtu au mnyama humchukua siku 2 hadi 21 kuonesha dalili za ugonjwa wa Ebola ambazo ni homa kali, Kuumwa kichwa, Kuharisha, Kutapika, Maumivu ya kifua, Maumivu ya tumbo, Mafua, Kikohozi, Maumivu ya misuli na viungo, hasa kwenye viungio, Kuvimba koo, Mwili kuwa dhaifu, Mfadhaiko, Kuchanganyikiwa, Macho kuwa mekundu, Kuvuja damu kwa ndani na nje.

Kwa Tanzania Wizara ya Afya tayari imetoa tahadhari ya ugonjwa huo wa Ebola na imetoa maelezo namna ambavyo watu wanaweza kujikinga na ugonjwa huo hatari.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola:

Epuka kugusa damu/majimaji ya wanyama ama binadamu walio na ugonjwa wa, Ebola au hata maiti za watu waliokufa kwa ugonjwa huo kwa kuzingatia haya, Tunza mazingira safi na salama ya hospitali, Watelekeze wagonjwa wa Ebola, Fukia miili ya waliokufa kwa Ebola kwa usalama, Epuka mazishi ya kienyeji kama kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola.

Watumishi wa afya na wanaowatazama wagonjwa wa Ebola wanatakiwa, Kuvaa kwa usahihi vifaa vya kujikinga na nyuso, mikono na macho, Na majoho maalum daima, Kutumia sindano mara moja na kuziteketeza ama kuzifukia, Epuka kutumia zaidi ya mara moja sindano au kutotumia sindano ambazo hazijachemshwa vyema, Epuka kuosha maiti za watu waliokufa kwa Ebola.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 19, 2019
Onyango azidi kuwa gumzo mitandaoni