Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa yasiyoambukiwa, Dr Neil Chapman wa Hospitali ya St Mary’s  amesema kuwa kawaida presha isiwe zaidi ya 140/90mmlHg.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na BHF taasisi ya uchunguzi wa mambo ya afya imesema kuwa presha ikiwa haitibiwi huharibu mishipa ya damu katika macho, misuli ya moyo kuwa minene na kusababisha mshtuko wa moyo ( heart attack), pia husababisha mishipa ya damu safi kuwa migumu na figo kushindwa kufanya kazi na kiharusi (stroke) ambapo mwisho wa siku husababisha vifo vya ghafla.

”Tatizo watanzania wengi hatuchunguzi afya zetu mara kwa mara, Watu wengi wanatembea na maradhi bila kufahamu na hicho ndicho chanzo cha vifo vya ghafla” amewahi kusema Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani  yasiyoambukizwa Dk Meshack Shimwela.

Lakini pia presha kwa mwanamke mjamzito inaweza kusababisha kifafa cha mimba  na kufanya hata kiumbe kufa tumboni, hivyo kuna sababu kubwa sana kwa mwanamke mjamzito na watu kuchunguza presha, kwani asilimia kubwa ya watu wazima hukumbwa na magonjwa yasiyoambukizwa kama vile presha.

Madaktari wamebainisha visababishi vya presha kuwa juu na kutaja pamoja na chumvi nyingi, unene uliozidi, umri mkubwa au uzee, figo ikishindwa kufanya kazi, kurithi na ugonjwa wa     kisukari.

Na dalili kubwa za mtu mwenye presha ni pamoja na kichwa kuuma, kizunguzungu, kubanwa na pumzi, kutokuona vizuri na kichefuchefu.

Pia vipo vitu vinavyochangia presha kuwa juu zaidi ni.

kula chumvi nyingi, unene uliozidi, kutofanya mazoezi, kunywa pombe nyingi na uvutaji sigara.

Kuepuka na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo kwa sasa yameshika kasi na yanasababisha vifo vya watu wengi zaidi na vingine vikiwa vya ghafla, kikubwa ni kufanya mazoezi, kula vyakula vyenye virutubisho vyote, kupunguza kutumia vyakula vyenya mafuta kwa wingi, kufanya mazoezi kila siku, kupunguza uzito uliopitiliza.

Wanasema kinga ni bora kuliko tiba hivyo ni vyema pia kuwa watu wa kuchunguza afya zetu mara kwa mara.

LIVE: Ziara ya Rais Magufuli mkoani Ruvuma
Video: Makonda atoa msaada wa milioni kumi kwa Wajane

Comments

comments