Mvutano wa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar umetoa picha rasmi ya vyama vya siasa ambavyo vimejiengua kushiriki na vile vitakavyochuana kwenye sanduku la Kura, Machi 20 mwaka huu.

Vyama tisa vya siasa kati ya vyama 14 vilivyoshiriki uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana vimetangaza kujitoa rasmi kwenye kinyang’anyiro hicho. Hivyo, vimeungana na msimamo wa chama kikuu cha upinzani visiwani humo, CUF.

Akitangaza uamuzi huo, Mratibu wa Umoja wa vyama hivyo, Kassim Bakalri ali alisema kuwa vyam hivyo vilipitisha maazimio ya kutoshiri uchaguzi huo baada ya kukutana Unguja.

Vyama hivyo vilivyoamua kujiengua ni UMD, Jahazi Asilia, Chaumma, UPDP, DP, CCK na ACT Wazalendo na CUF. Pamoja na vyama vya ADC na CCK ambavyo ushiriki wake una utata kutokana na wagombea wake kutangaza kushiriki huku uongozi wa vyama hivyo ukitoa msimamo wa kutoshiriki.

Chama cha CCK, kimetangaza kumsimisha uanachama mgombea wake wa urais, Ali Khatibu Ali. Uamuzi uliotangazwa kwa waandishi wa habari na Mwenyekiti wa chama hicho, Constatine Akitanda.

Wakati vyama hivyo vikisusia uchaguzi huo, vyama vya CCM, Tadea, TLP, SAU na AFP vimetangaza kushiriki na kuhimiza wapiga kura wake kujitokeza kwa wingi.

Mchungaji Msigwa aushangaa uamuzi huu wa Rais Magufuli
Serikali: Hatukuihonga mahakama