Corona ni virusi vinavyopatikana zaidi kwa Wanyama, lakini katika matukio machache virusi hivyo vinavyoitwa Zoonotic, Kisayansi, vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.

Virusi hivi vinaweza kuwafanya watu wakaugua, mara nyingi katika sehemu ya juu ya mfumo wa upumuaji sawa kabisa na mafua ya kawaida, ambavyo husambaa kutoka kwa Binadamu mmoja hadi mwingine kwa njia ya Hewa kwa Kukohoa au Kupiga chafya, Kugusana na mtu mwenye virusi hivyo

Njia nyingine ni Kugusa Kitu au sehemu yenye virusi na kisha kujigusa mdomo, pua au macho kabla ya kunawa na mara chache huambukiza kupitia kinyesi.

Dalili za kuwa umepata virusi hivi ni pamoja na Pua kudondosha mafua mfuulizo, Kuumwa Kichwa, Kukohoa, Kupata homa na muwasho katika Koo ila kwa wenye Kinga ndogo ya mwili kama wazee au watoto wanaweza kupata Nimonia (Pneumonia).

Video: Historia fupi ya marehemu Doglas, mwandishi TBC, ”Mwili uligundulika siku ya nne, ulianza kutoa harufu”

Hakuna Kinga ya Virusi hivyo kwa sasa, ila usambaaji wake kwa Binadamu unaweza kupunguzwa kupitia Kuosha mikono mara kwa mara kwa maji na sabuni na epuka kugusa macho, mdomo na pua kwa mikono isiyooshwa

Pia, unaweza kupunguza usambazaji wake kwa Kukaa mbali na mtu aliyethibitika kuwa na maambukizi. Ukianza kuona dalili hizo unashauriwa kumuona daktari

Ukithibitika kuwa na maambukizi ya Virusi hivyo, funika mdomo na pua yako wakati wa kupiga chafya au kukohoa na safisha sehemu au kitu ulichokigusa.

Kirusi hiki cha Corona, kinaaminika kuwa kilianza katika soko la bidhaa za baharini mwishoni mwa mwaka 2019, katikati ya Jiji la Wuhan, China ambalo lilikuwa linauza nyama ya porini.

Kirusi hiki kimeenea katika miji mingine ikiwemo Beijing na Shanghai, pia katika maeneo mengine duniani kama Marekani, Thailand, Korea Kusini, Japan, Australia, Ufaransa, Malaysia, Vietnam, Taiwan, Singapore, Nepal, Macau, Hong Kong na Canada.

Mpaka sasa kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kuwa, idadi ya watu wapatao 2045 wamegundulika kuwa na kirusi hiki huku.

324 kati ya hao 2045 wapo katika hali mbaya zaidi (critical condition) huku idadi ya waliokufa kutokana na kirusi hicho ikifikia 56 nchini China.

Hapo awali, China ilitoa tahadhari kuwa kirusi hiki kinaweza kusambaa kwa watu wengi zaidi.

Waziri wa Kamisheni ya Afya ya Taifa nchini China, Ma Xiaowei, akizungumza na vyombo vya habari, amesema kuwa, uwezo wa serikali wa kufahamu kirusi hiki kipya ni finyu na hawajui hatari zinazoweza kuambatana na kubadilika kwa kirusi hiki. [VOA]

Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona (Coronavirus) imekwisha fikia 106 hivi sasa kutoka idadi iliyoripotiwa mara ya mwisho ya 82.

Beijing, China imetangaza kifo cha kwanza kabisa katika jiji hilo kutokana na kirusi cha Corona, mwanamume wa miaka 50 aliyekuwa amesafiri kwenda Wuhan tarehe 8, Januari na kurejea jijini Beijing tarehe 15. Idadi ya vifo imefikia 82.

Kifo kingine kimeripotiwa kutokana na kirusi cha Corona katika mkoa wa Hainan nchini China. Hicho ni kifo cha kwanza kabisa katika mkoa huo. Jumla ya vifo kutokana na kirusi hicho ni 81 mpaka sasa.

 Idadi ya vifo nchini China kutokana na virusi vya Corona imeongezeka na kufikia 80 mpaka sasa huku idadi ya wenye maambukizi ikifikia zaidi ya 2700 ikijumuisha Hong Kong, Macau pamoja na Taiwan.

 

Malawi: Shule zafungwa kuhofia maandamano
Waziri atangaza maeneo waliyotenga kutibu watakao pata virusi vya Corona