Tumeona mahoteli mengi makubwa ambayo yanazingatia ulaji wa mlo kamili hupendelea kutoa huduma ya mayai kama kifungua kinywa, wengi wetu tumekuwa tukizani ndio kifungua kinywa pekee ambacho ni rahisi katika maandalizi yake.

Ndiyo, kwa watu wengine hufanya hivyo, lakini ni vyema kufahamu sababu nyingine muhimu katika afya ya mwili endapo mtu atafungua kinywa kwa kutumia mayai.

Japokuwa utafiti uliofanyika umebainisha kuwa ulaji mayai uliopitiliza huleta athari katika moyo, hivyo mtu anashauriwa atumie angalu mayai matatu kwa wiki.

Faida za kufungua kinywa na mayai hizi hapa.

1. Hutunza shibe
Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.

2. Husaidia kupunguza uzito
Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula.

3. Mayai ni chanzo kikubwa cha protini
Kama nilivyotangulia kusema kuwa mayai yana kiasi kikubwa cha protini kinachohitajika katika kujenga miili yetu. Hivyo basi ni vyema kula mayai asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho hivi.

Kumbuka hili ni sawa na kusema kuwa amino asidi zote muhimu tunazozihitaji katika mlo zinapatikana kwenye mayai.

4. Mayai hayaongezi lehemu (Cholesterol)
Ni dhahiri kuwa mayai yana kiwango fulani cha lehemu. Lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa lehemu iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye kiwango cha lehemu kwenye damu. Hivyo hakuna haja ya kuhofu juu ya magonjwa ya moyo yatokanayo na lehemu.

5. Husaidia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kumbukumbu
Kirutubisho kinachojulikana kama “Choline” kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu.

6. Hulinda macho
Kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara ya mionzi mibaya. Pia inaaminika kuwa zinazuia kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho uzeeni.

Kumbuka afya yako ni muhimu sana. Jali afya yako kwa kuzingatia ulaji bora wenye tija. Kumbuka kuwa huwezi kuwa na tija katika shughuli zako bila kuwa na afya njema. Badili mtazamo wako leo; tafuta mayai na ule kwa ajili ya afya yako.

Zitto asifu msimamo wa Serikali
Video: Mambo 6 usiyofahamu kuhusu Simba 'Mfalme wa nyika'

Comments

comments